Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wa Makao Makuu Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja katika maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi Duniani iliyofanyika katika Viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma tarehe 1 Mei, 2024
Maafisa wa Maadili kutoka Ofisi ya Rais,Sekretarieti ya Maadili Ya Viongozi wa Umma,Kanda ya Kaskazini-Arusha,Bw.Josephat Mkumbwa pamoja na Bi.Pendo Ulomi wakiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wapya wa Klabu ya Maadili iliyoko Arusha Girls Sec.School katika Halmashauri ya Jiji la Arusha wakati wa ufunguzi wa Klabu hiyo Tarehe 25 April, 2024.
Afisa Maadili kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Onesmo Msalagi akitoa mafunzo kwa wanachama wa klabu ya maadili ambao ni wanafunzi wa shule ya sekondari Mwananchi iliyopo Halmashauri ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma. Mafunzo hayo yalifanyika tarehe 24 Aprili 2024.
Bi. Rose Mugasha Afisa kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Ziwa akitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa uadilifu wanachama wa klabu za Maadili kutoka shule za msingi Nyasho A na Nyasho B wilayani Musoma Mkoa wa Mara. Mafunzo hayo yaliyofanyika katika shule ya msingi Nyasho A tarehe 15 Aprili 2024.
Afisa Uchunguzi kutoka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Kanda ya Kaskazini Bi.Asia Erasto akitoa elimu kwa Wanachama wa Klabu ya Maadili ambao ni wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kaloleni iliyopo katika Kata ya Kaloleni Jijini Arusha .Mafunzo hayo yalifanyika shuleni hapo tarehe 16 Aprili,2024.
Wanachama wa klabu ya Maadili ambao ni wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Nyanza wilaya ya Geita Mkoa wa Geita wakijengewa uwezo wa Maadili katika klabu yao na Bi. Abigail Majige kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Ziwa. Mafunzo haya yamefanyika tarehe 15 Aprili 2024 kwa klabu za Maadili zilizopo Shule za msingi na sekondari ndani ya Kanda ya Ziwa.
Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Kanda ya Kaskazini Bw. Gerald Mwaitebele akitoa elimu ya Maadili kwa wanachama wa Klabu ya Maadiil ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi Ukombozi iliyopo Kata ya Sokon Halmashauri ya Jiji la Arusha, wakati wa ufunguzi wa Klabu hiyo uliofanyika tarehe 9 April 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga akishuhudia Kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mhe. Fakii Lulandala, kilichoongozwa na Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini Bw. Gerald Mwaitebele. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara tarehe 05 Aprili 2024.
Baadhi ya maafisa uchunguzi kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakifuatilia mada mbalimbali zinatolewa wakati wa kikao kazi cha uchunguzi kilichofanyika ukumbi wa Ngorongoro jijini Arusha, tarehe 18 Machi 2024.
Kamishna wa Maadili, Jaji (Mst.) Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi akiongea na maafisa uchunguzi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika kikao kazi cha wachunguzi Kilichofanyika ukumbi wa Ngorongoro jijini Arusha tarehe 18 Machi 2024.