Kamishna wa Maadili awapa Kiapo cha Uadilifu Viongozi wakiwemo Majaji wapya wa Mahakama Kuu.


Kamishna wa Maadili awapa Kiapo cha Uadilifu Viongozi wakiwemo Majaji wapya wa Mahakama Kuu.
23
Apr
2018

Kamishana wa Maadili ya Viongozi wa Umma Mhe. Jaji (Mst) Harold Nsekela amewataka viongozi wakiwemo Majaji walioteuliwa hivi karibuni kufanya kazi kwa weledi na uadilifu mkubwa kwa kufuata kanuni na taratibu za nchi katika kuwatumikia wananchi.

Mhe. Nsekela ameyasemahayo tarehe 20 Machi, 2018 katika hafla fupi ya kuwaapisha Majaji kumi, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali na Naibu Mkurugenzi wa Mashtakailiyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam.

Aidha, Kamishna Nsekela amewaasa Majaji hao wapya kuwa kazi waliyopewa ni kazi nyeti inayohitaji Uadilifu wa hali ya juu zaidi, hivyo ni wakati sasa wa kuangalia marafiki gani ni wazuri na marafiki gani ni wabaya ili kuwawezesha kufanya kazi zao vizuri kwa kufuata kanuni na taratibu za nchi bila upendeleo wa aina yoyote.

“Kazi ya ujaji ni nyeti inahitaji umakini wa hali ya juu. Katika kazi hii, wapo marafiki mnaotakiwa kuwangalia upya. Marafiki wenye malengo yanayoenda kinyume na maadili yenu mnatakiwa kuwaacha,” alisema.

Kamishna Nsekela alisema, “Mtangulize Mwenyezi Mungu katika kutekeleza majukumu yenu ya kila sikuna kulinda Maslahi ya nchi na Taifa kwa ujumla.”

Naye Jaji Mkuu wa Tanzania Prof.Ibrahimu Khamisi Juma katika hotuba yake alifafanua kuwa, uteuzi wa Majajihao ulifuata vigezo vyote vinavyotakiwana kwamba ulishirikisha Wadau wote muhimu katika mchakato mzima wa kuwapata Majajihao.