Sekretarieti Ya Maadili Ya Viongozi Wa Umma Yapendekeza Kuanzishwa Sera Ya Maadili Ya Kitaifa


Sekretarieti Ya Maadili Ya Viongozi Wa Umma Yapendekeza Kuanzishwa Sera Ya Maadili Ya Kitaifa
09
Apr
2019

Sekretarieti Ya Maadili Ya Viongozi Wa Umma Yapendekeza Kuanzishwa kwa Sera Ya Maadili Ya Kitaifa

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inapendekeza kuanzishwa kwa Sera ya Maadili ya Kitaifa.

Mapendekezo hayo yametolewa na Kamishna wa Maadili Mh. Jaji (Mst) Harold R. Nsekela katika kikao cha siku ya pili cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika Jijini Dodoma.

Mhe. Kamishna wa Maadili ametoa wito kwa Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuwa wabunifu kwa kuanza kutafakari ni jinsi gani mdahalo wa kitaifa kuhusu sera ya Maadili utaweza kuanzishwa.

Aidha Mhe. Jaji Nsekela alifafanua kwamba Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma itashirikisha wafadhali au wadau wa maendeleo ili kuweza kuanzisha mdahalo wa Kitaifa kuhusu Sera ya Maadili ya Taifa ambayo itasaidia kusimamia na kukuza Maadili nchini.

Mhe. Kamishna katika hotuba yake amefafanua kuwa suala hili la uanzishwaji wa Sera ya Maadili ya Kitaifa unatakiwa uende sambamba na suala la nidhamu ya watumishi mahali pa kazi na kutambua sisi ni watu wa aina gani.

Mhe. Kamishna wa Maadili pia aliongeza kuwa ili Taasisi iweze kusonga mbele ni lazima watumishi kujiuliza “sisi kama watumishi tunaifanyia nini Taasisi na sio Taasisi inamfanyia nini mtumishi”.

Mhe Kamishna wa Maadili katika hotuba yake alieleza kuwa suala la matumizi ya TEHEMA katika Taasisi ni suala la kitaifa na haliepukiki aliwezikuepukika.Hivyo kila mtumishi anatakiwa kufanya kazi kuendana na teknologia ya TEHAMA. (Habari na Mawasiliano).