Watumishi Wa Maadili Watakiwa Kujitafakari Katika Utendaji Wao Wa Kazi


Watumishi Wa Maadili Watakiwa Kujitafakari Katika Utendaji Wao Wa Kazi
08
Apr
2019

Watumishi Wa Maadili Watakiwa Kujitafakari Katika Utendaji Wao Wa Kazi

Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wametakiwa kujitafakari kama wanayo Maadilina kama Wanafaa kuwa watumishi wa Ofisi hii nyetikulingana na matendo yao ikiwemo utendaji wa kazi.Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Maadili Mh. Jaji Mstaafu Harold R. Nsekela alipokuwa akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika tarehe 8 Aprili, 2019 katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma.

Aidha, Mh. Jaji Nsekela pia amewataka watumishi hao kujitafakari wenyewe katika utendaji kazi wao kupitia Idara na Vitengo vyao kuona kama wanatosha kuwa sehemu ya ofisi hiyo.Mh. Jaji Nsekela amefafanua kuwa mtumishi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma hapaswi kuhusishwa na vitendo vya uvunjifu wa maadili kwani atakuwa anakosa sifa ya kuaminiwa mbele ya jamii na Serikali kwa ujumla.Mhe. Jaji Nsekela katika hotuba yake amesema “Ni vema Watumishi Mtambue kuwa mmepewa majukumu nyeti, na pia mmebeba dhamana kubwa ya kuwezesha Serikali kutekeleza majukumu yake na ninyi ndiyo taswira ya Taifa letu kwa upande wa Maadili “watumishi wa taasisi hii hawatakiwi kutiliwa shaka katika uvunjaji wa maadili” alisema Mhe. Jaji Nsekela katika hotuba yake pia ameyataja baadhi ya masuala mbalimbali kufikia mwezi Machi, 2019 ambayo ni pamoja na kuhamia Makao Makuu ya nchi (Dodoma), kuanza kutumika kwa Muundo mpya na Mgawanyo wa Majukumu ya Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongoizi wa Umma baada ya kuidhinishwa na Mhe. Rais.


Aidha ameyataja masuala mengine ambayo Ofisi imeyatekeleza ikiwemo kuwezesha mafunzo mbalimbali ya muda mrefu na mfupi kwa ufadhili wa Serikali au Wadau wa Maendeleo kama vile Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AFDB) na (USAID,Mkoa wa Dar es Salaam kuna Kanda Maalumu ya Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inayosimamia Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar.Masuala mengine aliyotaja Mhe. Jaji Nsekela ni kuendelea na mchakato wa kuhamishia Makao Makuu ya Kanda ya Pwani katika mkoa wa Morogoro ambapo Kanda ya Pwani inasimamia Mkoa ya Morogoro na Tanga.

Mengine ni kushughulikia malalamiko dhidi ya ukiukwaji wa Sheria ya Maadili, kuratibu urejeshwaji wa Tamko la Raslimali na Madeni ambapo jumla ya Viongozi wa Umma 13,945 kati ya Viongozi 15,937 walirejesha Fomu za Tamko la Raslimali na Madeni kwa kipindi kinachoishia Desemba, 2018, kufanya Uhakiki wa Tamko la Raslimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma 594 kati ya Viongozi 2000 waliohakikiwa.

Ameyataja masuala mengine ambayo Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imefanikiwa kuyatekeleza kuwa ni kuratibu na kusimamia Hati ya Uadilifu ambapo Viongozi wakuu wa Kitaifa 63 walisaini Hati ya Uadilifu wakati walipoapishwa kushika nyadhifa mbalimbali za Uongozi.Mhe. Jaji Nsekela katika hotuba yake aliongeza kuwa katika kutekeleza agizo la Serikali la Makao Makuu ya Nchi kuhamia Dodoma, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilihamia rasmi Dodoma mwezi Januari, 2019, ambapo Ofisi zake zinapatikana katika Jengo la PSPF Tower, Barabara ya Jakaya Kikwete Ghorofa ya Saba.

Kikao hicho cha Baraza la Wafanyakazi ambacho ni cha Pili toka kuzinduliwa upya kwa Baraza hilo tarehe 4/5/2018 kimehusisha Wajumbe kutoka Makao Makuu na kwenye Kanda zote 8 ambazo ni Arusha, Dodoma, Mbeya, Mtwara, Mwanza, Tabora na Pwani na Dar es Salaam.